Watu wawili wauawa nyumbani kwa mgombea wa upinzani Chad


Watu wawili wameuawa baada ya vikosi vya usalama kwenda kumkamata mgombea wa upinzani Chad Yaya Dillo nyumbani kwake leo asubuhi. 


Dillo ambaye anapanga kugombea dhidi ya Rais Idriss Deby katika uchaguzi wa rais mwezi Aprili, amesema alishambuliwa nyumbani na walinzi wa rais na kuwa watu watano wa familia yake wameuawa, akiwemo mamake. 


Serikali imesema katika taarifa kuwa vikosi vya usalama vilikwenda nyumbani kwa Dillo kumkamata baada ya kupinga amri ya mahakama na wakakabiliwa kwa nguvu. Imesema watu wawili waliuawa na watatu wakajeruhiwa kutokana na tukio hilo. Huduma za intaneti zimekatwa katika mji mkuu N'Djamena tangu leo asubuhi. 


Dillo, kiongozi wa zamani wa waasi aliyepambana na Deby mwaka wa 2006 kabla ya kujiunga na serikali yake na kuwa waziri, amesema nyumba yake imezingirwa na vikosi vya serikali tangu tukio hilo la asubuhi.

Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items