Biden na Putin huenda watakutana mwezi Juni


Rais wa Urusi Vladimir Putin na mwenzake wa Marekani Joe Biden wanaweza kukutana mnamo mwezi Juni katika wakati mvutano unaongezeka kati ya Moscow na mataifa ya Magharibi. 

Taarifa hiyo ni kulingana na mshauri wa sera za kigeni katika ikulu ya Urusi, ambaye shirika la habari la taifa hilo RIA limemnukuu leo Jumapili. 

Hata hivyo afisa huyo, Yuri Ushakov amesema uamuzi wa mwisho kuhusu mkutano huo kati ya Biden na Putin bado haujafikiwa na Kremlin itazingatia masuala kadhaa kabla ya kufanya uamuzi. 

Mapema mwezi huu rais Biden aliitaka Urusi kusitisha shughuli zake za kijeshi kwenye mipaka ya Ukraine na kupendekeza kufanyika mkutano kati yake na Putin ili kutafuta majibu ya masuala yanayoleta misuguano baina ya pande hizo mbili.

Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi