Jeshi la Israel lawakamata Wapalestina 13


Jeshi la polisi la Israel limewakamata Wapalestina 13 katika maeneo tofauti ya Jerusalemu Mashariki ,eneo lililokaliwa kimabavu na Israel.

Katika habari iliyochapishwa na wakala rasmi wa Palestina WAFA, ilielezwa kuwa polisi wa Israeli walivamia nyumba nyingi katika sehemu tofauti za Mashariki mwa Jerusalem, haswa katika Jiji la Kale ambako kuna Masjid al-Aqsa.

Ripoti hiyo, kwa kuzingatia mashuhuda wa macho, ilisema kuwa Wapalestina 13 walikamatwa na polisi wa Israel wakati wa uvamizi huo.

Hakuna taarifa bado iliyotolewa na polisi wa Israel kuhusu mahabusu.

Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi