Tawasifu ya Rais wa pili wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Ali Hassan Mwinyi, iitwayo 'Mzee Rukhsa: Safari ya Maisha Yangu' itazinduliwa Leo tarehe 8 Mei 2021 katika ukumbi wa JNICC Dar es Salaam
Kitabu hiki kimebeba simulizi za maisha yake binafsi na safari yake ya uongozi, hadi kinakamilika kimegharimu Tsh Milioni 190.
Mgeni rasmi katika uzinduzi huo anatarajiwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu_Hassan