Serikali ya Tanzania imefungia laini za simu 18,622 baada ya kubainika kufanya matukio ya uhalifu nchini.
Hayo
yamesemwa na Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dk Faustine
Ndungulile leo Jumatano Julai 28 2021 wakati akifungua mkutano wa
mapato na matumizi wa wizara na taasisi zake.
Amesema kuwa
laini hizo ziligundulika katika kipindi cha kati ya Aprili hadi Juni
mwaka huu na kuwataka Watanzania kuhakiki usajili wa laini zao.
“Tumevizuia
vitambulisho vilivyotumika kusajilia laini 14,768, ndio maana niwaombe
sana Watanzania tuendelee kufanya uhakiki wa laini zetu ili hayo yasije
yakajitokeza,”amesema.
Amesema watu wamekuwa wakisajiliana laini za simu kwa kutumia vitambusho vya wengine.
