Rais Joe Biden kuandaa mkutano wa masuala ya demokrasia

 


Ikulu ya White House nchini Marekani pamoja na wizara ya mambo ya kigeni zimetangaza kufanyika kwa mkutano wa kilele uliosubiriwa kwa shauku Disemba mwaka huu. 

Mkutano huo wa kilele ni utekelezaji wa ahadi ya Biden ya kuwaleta pamoja wakuu wa mataifa ya ulimwengu ili kuongeza nguvu ya mapambano ya kiitikadi wakati ulimwengu ukipambana na mzozo wa utawala wa kiimla. 

Wakati mkutano huo uliopangwa kufanyika Disemba 9 na 10 mwaka huu utakaofanyika kwa njia ya mtandao kutokana na janga la COVID-19 rais Joe Biden atafuatilia kwa kuzungumza na wakuu hao kibinafsi Disemba mwaka 2022. 

Wizara ya mambo ya kigeni imesema lengo hasa ni kujenga msingi wa ushirikiano kuelekea kuijenga upya demokrasia ya ulimwengu.


Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi