Na Timothy Itembe Mara.
Wanafuniz wameaswa kujenga utamaduni wa kudumisha Amani na kuondoa tabia ya migogoro pindi wanapokuwa mashuleni ili kufikia malengo.
Mkuu wa Shule ya sekondari Tarime,Machota Kora alisema tumekuwa tukisikia migogoro mingi mashuleni watoto wakigoma hata wengine wakichoma mashule na mabweni napenda kutumia nafasi hii kuwaonya wenye tabia kama hiyo waache mara moja na kuzingatia kilichowapeleka kusoma.
Mafanikio mengi ya kimaisha na ufaulu mashuleni vinakuja baada ya wanafunzi kujitambua na kujenga tabia ya nidhamu huku wakiepuka migogoro badala yake wajibidishe na masomo na kuzingatia kilichowapeleka mashuleni huku wakihurumia Wazazi na walezi wanaotoa gharama zao kuwasomeasha ili wafikie malengo kwa maisha ya baadaye aliongeza kusema Kora.
"Malengo ya wanafunzi na walimu yanashindwa kufikiwa pindi midhmu inapokuwa imepungua kati ya wanafunzi,walimu na wazazi ikiwemo jamii inayowazunguka ambapo maswala mengi yanakuwama kufikiwa kutokana na midhamu shirikishi kupungua kwa mwaka huu shule yetu imejipanga kufanya vizuri na kuwa kati ya shule kumi Bora kitaifa mwaka ujao baada ya kurekebisha kasoro zilizo kuwepo"alisema Kora.
Mwalimu huyo alibainisha kuwa shule yake kwa miaka iliyopita ufaulu ulikuwa chini lakini baada ya kurekebisha kasoro zilizokuwepo ikiwemo nidhamu kwa wanafunzi,ushirikianomkazini pamoja na uongozi kubadilishwa ndani ya miaka mitatu mfululizo 2019-2021 matokeo ya ufaulu wa mitihani wamefanya vizuri kitaifa na haijashuka ufaulu.
Kora aliongeza kusema mafanikio hayo yamekuja baada ya shule yake kuondoa migogoro iliyokuwepo baina ya jamii kutoshiriki katika shuguli za maendeleo ambapo kwa ujumla sasa wanashiriki na Wanafunzi wamejenga nidhamu,walimu pamoja na jamii inayowazunguka pamoja na kufanya mabadiliko ya uongozi lengo likiwa kutaka mabadiliko ya kufikia ufaulu.
