F Waasi wa Tigray wapora vifaa vya misaada | Muungwana BLOG

Waasi wa Tigray wapora vifaa vya misaada


 

Vikosi vya mkoa wa Tigray nchini Ethiopia vimefanya uporaji kwenye hifadhi za misaada ya kibinadamu ya Marekani katika mkoa wa jirani wa Amhara.Ripoti zinaeleza

Vikosi hivyo havijasema chochote kuhusu madai hayo.

Mkuu wa shirika la misaada la Marekani USAID nchini Ethiopia ameiambia televisheni ya serikali kuwa wapiganaji wa Tigray wamepora hifadhi yote ya misaada, wamechukua vyakula na vifaa vingine. Pia wameiba magari, aliongeza.

Amesema pia wamefaya ''uharibifu mkubwa '' katika vijiji walivyokwenda.

Juma lililopita, maafisa mjini Amhara walivishutumu vikosi Tigray kwa mauaji ya raia 40 na kuharibu shule, hospitali na vifaa vingine.

Vikosi vya Tigray, ambavyo vimekuwa vikipambana na vikosi vya shirikisho na washirika wake kwa miezi 10, vimepeleka vita hivyo nje ya ardhi yao, na kuingia mikoa ya jirani ya Amhara na Afar.

Wameunda umoja na kundi la waasi katika jimbo kubwa nchni humo la Oromia, unaotishia sehemu kubwa ya Ethiopia.

Post a Comment

0 Comments