Oct 13, 2021

Zifahamu faida za kula njegere kiafya

  Muungwana Blog 2       Oct 13, 2021

 Njegere ni mboga yenye virutubisho vingi vinavyofanya kazi ya kujenga mwili, kuboresha ufanyaji kazi wa ini na ni chanzo kizuri cha Protini.

Ulaji wa njegere mara kwa mara husaidia kuboresha kinga ya mwili, hurekebisha kiwango cha sukari kwenye damu lakini pia huzuia mtu kuzeeka kwa haraka na zina kiwango kidogo cha kalori.

Njegere zina kiwango kikubwa cha nyuzinyuzi, vitamin A,B, na C na hazina mafuta yanayoweza kuganda katika mishipa ya damu.

Lakini pia zinauwezo wa kuzuia saratani ya tumbo.

Protini iliyopo katika mboga hii husaidia kuyeyusha damu iliyoganda na kwa wagonjwa wenye upungufu wa damu, wanatakiwa kutumia njegere zilizochemshwa kila siku.

Ulaji wa njegere za kijani huongeza damu, hukabiliana na udhaifu wa afya lakini zinasaidia kupunguza maumivu katika kidonda kinachouma kwa sababu inasaidia kuondoa asid zilizopo tumboni.

Utafiti uliofanywa na mtaalamu wa tiba-lishe wa taasisi moja nchini Marekani, Dk.George Mateljan anasema, njegere ni miongoni mwa vyakula vyenye kiwango kikubwa cha kamba lishe zenye uwezo wa kushusha kiwango cha lehemu inayosababisha shambulio la moyo.

Matokeo ya utafiti wake huo aliouandikia kitabu kiitwacho The World’s Healthiest Foods, Dk Mateljan anasema asilimia 65 ya mbegu ya njegere ni kamba lishe ambapo pamoja na kushusha lehemu, pia huondoa shinikizo ya damu na kuzuia shambulio la moyo. “Watu wengi wanakula kidogo sana, hawajui faida hizi.

Lakini ukweli ni kwamba njegere ni chakula muhimu mwilini hasa kwa wagonjwa wa moyo na sukari,” alisema Dk Mateljan na kuungwa mkono mtaalamu mwingine Dk Rafael Nyampiga wa jijini Dar es Salaam

logoblog

Thanks for reading Zifahamu faida za kula njegere kiafya

Previous
« Prev Post

No comments:

Post a Comment