Hamdok asema alirejea kwenye wadhifa wake Sudan ili kulinda mafanikio ya kiuchumi


Waziri Mkuu wa Sudan Abdalla Hamdok amesema kuwa kudumisha mafanikio ya kiuchumi yaliyopatikana katika miaka miwili iliyopita ni miongoni mwa sababu zilizomfanya akubali kurejea katika wadhifa wake, chini ya makubaliano na jeshi karibu mwezi mmoja baada ya kuondolewa kupitia mapinduzi. 


Katika mahojiano na shirika la habari la Reuters kwenye makazi yake mjini Khartoum ambako amekuwa chini ya kifungo cha nyumbani kufuatia mapinduzi ya kijeshi ya Oktoba 25, Hamdok amesema anaamini kuwa serikali ya wataalam itakuwa na fursa ya kuboresha viwango vya maisha ya watu. 


Vyama maarufu vya kisiasa na vuguvugu lenye nguvu la maandamano nchini Sudan wamepinga uamuzi wa Hamdok kusaini makubaliano na jeshi jana, huku baadhi wakisema ni mbinu ya kisiasa ya kuyafunika mapinduzi yaliyofanywa.

Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi