India, Urusi na China zimesema Afghani ni eneo la maovu


Mawaziri wa mambo ya nje wa India, Urusi na China wameonesha wasiwasi wao juu ya kuzorota kwa hali ya kiutu nchini Afghanistan na ongezeko la kusambaa kwa dawa za kulevya.


Katika taarifa ya pamoja baada ya mkutano wao kwa njia ya video baina ya waziri Subrahmanyam Jaishankar wa India, Sergey Lavrov wa Urusi na Wang Yi wa China wametoa wito wa haraka wa msaada wa kibinaadamu pasipo vizuizi vyovyote.


Pamoja na mataifa hayo mawili kutoa ahadi ya kukabiliana na magendo ya biashara ya dawa za kulevya wameitaka mamlaka ya Taliban kuheshimu matokeo ya maazimio ya Umoja wa Mataifa na jumuku lake muhimu kwa taifa hilo.


Afghanistan ilitumbukia katika mgogoro mwezi Agosti baada ya kusitishwa msaada wa kigeni, kulikotokana na kuporomoka kwa serikali iliyokuwa inaungwa mkono na mataifa ya magharibi na kurejea madarakani kwa Taliban.

Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi