Mataifa wanachama wa WHO wanakutana kujadili kujiandaa na majanga


Mataifa 194 wanachama ya Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO) wanatarajiwa kukutana leo hii, zingatio likiwa kutafakari pendekezo la kuboresha hali ya dunia kujiandaa na janga lijalo.Mawaziri wa mataifa wanatajadili iwapo waanze majadiliano rasmi ya makubaliano ya janga au la. 


Jana Jumapili katika ukurasa wake wa Twitter, ubalozi wa Ujerumani nchini Geneva uliandika mataifa yatapaswa kukubaliana kuhusu rasimu ya uamuzi ambao utazindua majadala wa majadiliano na kisha kuwekewa muda maalumu.


Uamuzi wa rasimu unatarajiwa kuidhinishwa katika siku tatu za kikao cha WHO, kinachoanza Jumatatu. Mataifa ya Umoja wa Ulaya ni miongoni mwa yake ambayo yanatajwa kuachwa na makubaliano ya kimataifa ya kuhusu janga, lakini Marekani na China zinaonesha mashaka na kuwepo kwa lolote jipya katika ahadi nyingi zilizotolewa.

Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi