Nyara za Serikali zanaswa Tarangire

 


Kikosi maalumu cha kupambana na ujangili katika eneo la ikolojia ya hifadhi ya Taifa ya Tarangire na Manyara kimemkamata meno mawili ya tembo baada ya kufanya upekuzi katika nyumba ya mtuhumiwa wa ujangili.


Uchunguzi uliofanywa na mwananchi na kuthibitishwa

 Kamanda wa Kikosi cha Kuzuia Ujangili (KDU) Kanda ya Kaskazini, Peter Mbanjoko ameithibitishia Mwananchi kuwa meno hayo yamekamatwa Kijiji cha Kakoi wilayani Babati mkoa wa Manyara.


"Ni kweli Kikosi cha kupambana na ujangili ambacho kinahusisha askari wa Taasisi ya Wanyamapori (TAWA) askari wa Hifadhi ya Tarangire, askari ya Burunge WMA na wa Taasisi ya Chemchem iliyowekeza katika eneo hilo ndio wamefanikisha kukamatwa meno hayo"amesema


Amesema mtuhumiwa alikimbia kabla ya kutiwa mbaroni na bado anasakwa lakini huku wakimshikilia mke wa mtuhumiwa kwa mahojiano.


Tukio hili kimetokea siku chache baada ya kukamatwa mtuhumiwa mwingine akiwa na nyama ya pundamilia, ngozi na mkia na kabla ya tukio hilo watuhumiwa wengine wanne walikamatwa na meno  ya tembo.


Meneja wa Taasisi ya Chemchem, Walter Pallangyo amesema kuendelea kukamatwa kwa watuhumiwa kunatokana na kuimarishwa  operesheni.


Amesema kuongezeka shughuli za kibinaadamu katika maeneo ya hifadhi na mapito ya wanyama imekuwa chanjo cha kuendelea ujangili.


"Uvamizi mkubwa maeneo ya hifadhi na mapito ya wanyama unaoendelea tunaomba Wizara ya Maliasili na Utalii kukamilisha mchakato wa kuweka mipaka lakini pia kutengwa maeneo ya hifadhi na shughuli nyingine"amesema.

Post a Comment

0 Comments