Ticker

6/recent/ticker-posts

 


Rasilimali saba (7) ambazo ukizitumia leo zitakupa mafanikio

 Moja ya changamoto kubwa itukumbayo watu wengi ni ile hali tunayoshindwa kutumia vizuri rasimali tulizonazo. Wengi huwa tunazichukulia ya kwamba rasilimali tulizonazo si kitu katika kutuletea mafanikio. Lakini ukweli ambao upo wazi ni kwamba rasilimali ni zawadi pekee ambayo ni zawadi tosha kwetu sisi kuweza kufanikiwa.

Swali la msingi ni je tunazitumiaje rasilimali hizo kuwa fursa za kimafanikio ? Hapo ndipopalipo na changamoto kwa watu wengi. Na daima ukubukwe ule usemi mzuri usemao “Kuzaliwa  Masikini si Kosa ila Kosa ni wewe kufa Maskini”, na  kufa kwako maskini inategemea sana kwa kutokutumia vizuri Rasilimali  zifuatazo.

1. Uhai
Katika zawaidi na rasilimali kubwa ambazo mwenyezi Mungu amekutunuku ni pamoja na uhai. Uhai ndiyo zawaidi pekee ambayo ni vyema ukaitumia vyema katika maisha yako. Rasilimali hii ndiyo ambayo kila mmoja wetu anapidi aitumie vyema katika kubadili maisha yake. Kwanini ufe maskini na ili hali wewe u hai? Tafakari kisha tafuta majibu ya maswali yako.

Uhai huu tulionaona hatuna budi tuutumie vyema, kwani mwenyezi Mungu ana makusudi ya dhati nasi. Mwenyezi Mungu katupa uhai huu pasipo kutumia hata shilingi moja. Kama ndivyo hivyo naomba utafakari tena ni kwanini ufe maskini? . Uhai ulionao hakikisha unafanya kitu ambacho kitaacha alama duniani kote kabla hujarudi mavumbini.

2. Muda
Muda ni rasilimali nyingine ambayo itakufanya wewe uweze kufikia ndoto yako endapo utaamua kutumia vyema muda ulionao. Katika hili ni vyema ukatenga kwa kila siku walau saa moja ambalo litakufanya uweze kufikiri ni jinsi gani utawwza kufikia vyema ndoto uliyonayo. Muda ni rasilimali kubwa sana ambayo watu wenye mafanikio huweza kuutumia kama silaha dhidi ya umaskini.

3. Akili.
Kila mwanadamu katika ulimwengu huu ana akili. Na akili hizi ndizo ambazo humtofautisha mtu mmoja na mwingine. Akili ni njia ambayo itakufanya uweze kutimiza kusudio lako la kuwepo duniani hapa. Akili ndiyo rasimali tosha inayomfanya mtu afikiri nini afanye na nini asifanye. Hivyo nikusihi ifanye akili iweze kufikiri kabla ya kutenda, kwani changamoto kubwa ambayo inawafanya watu waweze kuwa maskini ni vile mtu anavyoamua "kutenda bila kufikiri" au "kufikiri bila kutenda'.

4. Nguvu.
Nguvu uliyonayo itumie vyema katika kutenda kazi mbalimbali. Lakini kutenda huku si kutenda tu, la hasha bali ni kutenda kwa bidii. Kufanya kazi bila kuonyesha juhudi za maksudi ni sawa na bure.

5. Kipaji/ talanta
Rasimali nyingine uliyonayo unayoweza kukufanya uweze kufanikiwa ni  kipaji. Watu wengi wenye mafanikio waliweza kutumia kipaji kwa asilimia kubwa, na leo tumeshuhudia ya kwamba mafanikio yamekuwa upande wao. Hivyo tumia talanta kama sehemu ya kukutoa sehemu moja kwenda sehemu nyingine.

Je kipaji ulichonacho kinakusaidia? Kama jibu ni hapana basi endelea kusoma mahali hapa kwani siku sijazo nitakueleza jinsi ambayo utaweza kugeuza kipaji hicho kuwa pesa.

6. Ardhi
Ardi pia ni sehemu ya maisha yako, kila kitu unachokitaka kukifanya lazima kiwe na mahusiano ya karibu na ardhi. Tafakari kwa umakini juu ya ardhi hii kisha uone fursa lukuki ambazo zimejificha katika ardhi, fursa hizo lukuki  zitakusaidia kuweza kufanikiwa katika maisha yako.

7. Watu
Rasimali ya mwisho ambayo tutaijadili siku ya leo, ni kuhusu watu ambao wanakuzunguka. Kila kitu huwezi kufanya kitu bila kushirikisha watu. Kama ni biashara inahitaji wateja, kama ni shule inahitaji wanafunzi, kama ni kanisa au mskiti nalo linahitaji watu pia. Hivyo ni vyema ukaweza kuwatumia watu mbalimbali kuweza kufikia lengo lako. Kama unataka mfanyabishara tunachotegemea kuona kwako ni kuona rafiki zako wakubwa ni wafanyabishara wanzako.

"Kwani kuna usemi unao sema tutajie rafiki zako tujue tabia zako"

Hivyo hakikisha unazungukwa na marafiki wenye tija kila wakati.

Bila shaka umenielewa vizuri, kama umeshindwa kutumia rasimali hizi basi endelea kusubiria kupanda ndege kituo cha daladala. Endelea kutembelea Muungwana blog kila wakati.

Na. Benson Chonya

Post a Comment

0 Comments