RC Telack awataka maofisa utumishi kuwahudumia walimu haraka.


Na Ahmad Mmow, Lindi. 

Katika kuhakikisha walimu mkoani Lindi wanatumia muda mwingi kufundisha. Mkuu wa mkoa wa Lindi, Zainab Teleck amewataka maofisa utumishi wa halmashauri katika mkoa wa Lindi kuwahudumia walimu haraka wanapohitajihuduma. 


Telack ametoa agizo leo katika viwanja vya shule ya Mpilipili, manispaa ya Lindi  wakati wa uzinduzi wa siku ya mwalimu wa darasa la kwanza. 


Telack ambae alikuwa mgeni rasmi katika ghafla hiyo ambayo ilikuwa ya ngazi ya mkoa alisema serikali inatambua, kuthamini na kuheshimu kazi inayofanywa na walimu Kwahiyo nilazima waheshimiwe na kuhudumiwa  haraka. 


Mkuu huyo wa mkoa wa Lindi ambae pia aliwataka walimu walinde na kutunza heshima ya kazi ya ualimu alisema asingependa kuona walimu wanakaa au kusimama kwa muda mrefu kwe misururu bila kuhudumiwa. Kwani kitendo cha kuwachelewesha kinasababisha wapoteze muda ambao wangetumia kufundisha. 


 " Watu wathamini na kuheshimu kazi ya ualimu. Heshima ya walimu irudi kwenye nafasi yake," Teleck alisisitiza. 


Katika kudhihirisha kwamba serikali ya mkoa huu inathamini na kutambua umuhimu wa walimu, mkuu huyo wa mkoa alisema mkoa umejipanga kujenga nyumba za walimu. Kwani nia ya serikali nikuona walimu wanafanya kazi kwa furaha, amani na utulivu. 


Sambamba na hayo, amewataka maofisa utumishi kuwapandisha madaraja walimu. Huku akionya kwamba upandishaji huo uzingatie taratibu na sheria. Kwani nijambo lisilo kubalika kuona au kusikia mwalimu ambae anamuda mfupi kazini tangu aajiriwe anapandishwa madaraja haraka na kuwaacha aliowakuta wameajiriwa kabla yake. 


Kwa upande wake ofisa elimu wa mkoa wa Lindi, Vicent Kayombo alisema idara ya elimu mkoani humo imejipanga kuhakikisha watoto wa darasa la kwanza wanajua kusoma, kuandika na kuhesabu (KKK) kabla ya mwezi Juni kila mwaka. 


Katika kuhakikisha mpango huo unafanikiwa Kayombo alisema walimu wa darasa la kwanza watapata mafunzo katika chuo cha ualimu Nachingwea ili kuwaongezea weledi. 


Uzinduzi huo ulitumika pia kukabidhi zawadi kwa watoto wa darasa waliofanya vizuri shindano la kusoma, kuandika na kuhesabu  lililofanyika 28.9.2021. 


Ambapo Yakubu Yahya alikuwa kutoka shule ya msingi Majengo halmashauri ya Nachingwea alikuwa wa kwanza, Sara Mohamed Nanjia wa shule ya Ruangwa halmashauri ya wilaya Ruangwa alikuwa wa pili na  Benjamin Samuel wa shule ya msingi Singino  halmashauri ya wilaya ya Kilwa alishika nafasi ya tatu

Post a Comment

0 Comments