https://monetag.com/?ref_id=TTIb Taiwan: Ulaya lazima ilinde demokrasia kwa pamoja | Muungwana BLOG

Taiwan: Ulaya lazima ilinde demokrasia kwa pamoja

 


Rais Tsai Ing-wen wa Taiwan leo hii ameuambia ujumbe wa wabunge kutoka mataifa ya Baltic kwamba taifa lake na Ulaya lazima zishirikiane katika kujilinda dhidi ya uimla na upotoshaji.


Akizungumza na wabunge kutoka mataifa ya Lithuania, Latvia na Estonia walioko ziarani nchini humo Rais Tsai alisema demokrasia wanayoifurahi kwa sasa ilipatikana kwa tabu sana, jambo ambalo wote wanalielewa.


Tangu ikubali kufungua ubalozi wake nchini humo, Lithuania imekuwa ikikabiliwa na shinikizo la muda mrefu kutoka kwa China, ambayo inadai Taiwan ni sehemu yake. 


Hadi sasa hakuna taifa mwanachama la Umoja wa Ulaya ambalo limetangaza kuwa na mahusiano rasmi na Taiwan

Post a Comment

0 Comments