Tasac yafanya mkutano wa kuwahimiza wasafirishaji kujiunga na baraza la usafirishaji


Na Maridhia Ngemela, Mwanza.

wadau mbalimbali wa usafirishaji wamekutana Jijini Mwanza  leo hii katika  mkutano wa uhamasishaji ulioandaliwa na baraza la usafirishaji Tanzania (TSC) kwa kushirikiana na Shirika la uwakala wa meli Tanzania (TASAC) wenye lengo kujadili  mambo mbalimbali ya uboreshaji wa sekta ya uchukuzi.

Lengo la mkutano huo ilikuwa Ni kupata uzoefu kutoka kwa wataalam ili kubadirishana ujuzi na uzoefu utakaowajenngea uwezo mkubwa na kujiamini katika kazi za usafirishaji shehena kupitia usafiri majini.


Akizungumza katika mkutano huo Meneja huduma za bandari Julius Mitinje ameeleza lengo la mkutano huo ni  kuendeleza ushirikiano Kati ya mdhibiti na wadau wa sekta inayodhibitiwa na Tasac kama njia moja wapo ya kuinua uchumi kupitia sekta ya usafiri majini na kuchagiza uwezo wa wasafirishaji shehena nje ya Nchi kupitia usafiri majini ili waweze kufanya biashara yao kwa ufanisi.

Amesema tija ,ufanisi na mafanikio ya wasafirishaji shehena nje ya Nchi vinaathiri na kuathiriwa na watoa huduma mbalimbali katika sekta ya usafirishaji kwa njia ya maji hivyo ni muhimu kwa sekta inayodhibitiwa na Tasac .

" Usafirishaji shehena kimataifa kwa njia ya maji ni  muhimu sana kwa Tasac na watoa huduma wanaodhibitiwa na Tasac  bandari zetu ni kupakia na kupakua shehena inayomilikiwa na wasafirishaji meli zinazokuja kwenye bandari zetu kufuata shehena za wadau ,wakala wa ugomboaji shehena ,bandari kavu hivyo ufanisi wa wasafirishaji shehena ni suala muhimu kwa Tasac na watoa huduma sekta ya usafiri majini amesema Mitinje.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa baraza la usafirishaji shehena Tanzania Ashraf Khan alipokuwa akifanya mahojiano na waandishi wa habari amesema kuwa, wasafirishaji wapatiwe elimu juu ya kuwa na nyaraka muhimu kabla ya usafirishaji mizigo,ununuzi ilikuondoa usumbufu bandarini na Mamlaka ya mapato Tanzania.

Khan amesema changamoto za ukuaji wa mizigo pamoja na taratibu zilizofanyika kwa upanuaji wa bandari bado shehena nikubwa sana.

Amesema mategemeo yao bandari ni kuwa na tani million elf 20,000 kwa mwaka huu kutokana na Hali ya usafirishaji kuzidiwa kutokana na kupata meli za sarifa upande wa bandari zenye tani elfu 30,000.

Naye Program Menager -shipping ,ports& Freight services Aderick Kagenzi ameongeza kuwa, Katika tafiti zao wamebaini kuongeza uboreshaji,utendaji wa bandari na kuondoa vikwazo vya Kati ili bandari ya Dar es salaam iendelee kuwa lango kuu la bandari Africa Mashariki na Kati.

Akizungumzia upande wa tozo amesema kuwa Katika bandari siyo kubwa kwani wanaangalia namna ya kutoza tozo hizo kulingana na hali ya uchumi.

Amesema kuwa msafirishaji ili asafirishe mzigo wake ni lazima aangalia unafuu wa safari ya kusafirisha mzigo, kwa kuangalia muda, usalama na ndio maana mizigo mingi inapita Bandari ya dar es salaam kutokana na uelekeo wa mzigo unapoenda.

Kagenzi ameongeza kuwa Serikali iendelee kufanya maboresho zaidi hususani kuondoa vikwazo mbalimbali vinavyo kwamisha mizigo kusafirishwa kwa wakati katika bandari ya Dar es salaam hali itakayosaidia utendaji kazi kuwa wenye tija.

 Miongoni mwa wasafirishaji waliohudhuria mkutano huo ni Moses Kidege kutoka  S.H.Amon ameomba elimu izidi kutoelewa kwa wasafirishaji ili  wawe na uwelewa zaidi katika kazi hiyo ya usafirishaji kwani wanakutana na changamoto mbalimbali ambazo wakipatiwa elimu watapata ufumbuzi zaidi.

 Mwenyekiti wa Chama cha wavuvi Tanzania (Tafu) Bakari Kadabi amesema kuwa,kupitia mkutano huo wamepata kufahamu sheria ambazo zitazidi kuwaongoza katika usafirishaji wa mizigo ambayo wanaitegemea kukuza uchumi wa familia na Nchi kiujumla.

 

Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi