Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani kuzuru Kenya na Nigeria

 


Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken atafanya ziara yake ya kwanza rasmi barani Afrika wiki ijayo, akizuru Kenya, Nigeria na Senegal.


Wizara ya Mambo ya Nje ilisema Bw Blinken atakutana na marais wa nchi zote tatu, na kutoa hotuba kuhusu sera ya Marekani na Afrika.


Katika hatua ya kwanza ya ziara yake - nchini Kenya - anatarajiwa kujadili masuala ya usalama wa kikanda kama vile Ethiopia, Somalia na Sudan. Majadiliano mapana yanatarajiwa kujumuisha mabadiliko ya tabia nchi na kumaliza janga la Covid-19.

Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi