Ticker

6/recent/ticker-posts

 


Madiwani waibana Tarura Mji wa Tarime


Na Timothy Itembe Mara

Wakala wa Barabara mjini na vjijijibi TARURA wamebanwa na Madiwani wa halmashauri ya Mji wa Tarime kwa lengo la kutaka kujua ubora wa barabara zinazolimwa na kuwekewa lami katika halmashauri yao


Diwani Viti maalumu kata ya Nyandoto Dorisi Maxmiliani Chacha kwa niaba ya wenzake aliuluza swali la kutaka kujua ni lini barabara za halmashauri ya Tarime mjini zitalimwa kwa kiwango na wananchi wakapata kutembea na kupita kwa urahisi bila kusumbuka.


Diwani huyo aliongeza kusema Barabara zilizopo hazipitiki na nishida kwa wasafiri wa miguu na vyombo vya moto kwa hali hiyo wasafiri wanasumbuka kwa kulipishwa na kutozwa gharama kubwa ya nauli kwa baadhi ya maeneo ya karibu kutokana na ubovu wa barabara.


Diwani huyo alitaka Barabara zilizopo ziboreshwe ili wasafiri na watumiaji wa vyombo vya usafiri wapate kunufaika kwa ubora utakao kuwepo pamoja na gharama ya nauli kupungua.


Naye Chacha Marwa Machugu (maarufu Chacha msukuma) alitaka kujua nilini barabara za kata ya Tutwa zitalimwa huku zikiboreshwa  na  wasafiri,watembea kwa miguu wapate kupita kwa urahisi hususani wafanya biashara wanaoleta biashara zao katika soko la Rebu.


Akitolea mfano barabara itokayo kwa Marehemu mkuu wa majeshi Mwita Kiaro kuelekea Rebu sekondari hadi Rebu sokono alisema barabara hiyo ni mbovu na haipitiki kwa kurahisi na kuongeza kuwa barabara hiyo nilini itarekebishwa na kuboreshwa maeneo korofi ili wafanyaboashara ikiwemo wanafunzi kupita kwa raha.


Kwa upande wa Diwani kata ya Kenyamanyori Farida Joel alitaka kujua vigezo wanavyotumia wataalamu wa Tarura kubaini maeneo korofi.


Diwani huyo aliongeza kuwa barabara nyingi zina maeneo korofi lakini cha ajabu wanasomewa kuwa Tarura inarekebisha maeneo hayo ambayo kwa nafasi yake alipata kigugumiozi kuhusu maeneo yanayorekebishwa kwa maana ya maeneo korofi.


Farida aliomba Tarura kutendea wananchi wa kata yake haki kwa kulima na kurekebisha maeneo korofi ya barabara ambayo yanalalamikiwa na wananchi wa Kata yake ikiwemo barabara za halmashauri ya Mji wa Tarime kwa ujumla  kuboreshwa na kuondoa sintofahamu inayoweza kuwakwamisha kipindi cha mchakato wa kupiga kura za uchaguzi.


Mwenyekiti wa halmashauri ya Mji wa Tarime Daniel Komote aliwaomba watu wa Tarura kubainisha BOQ hususani kazi gani zitafanyika na mkataba utaisha lini ili kuondoa mkanganyiko baina ya Madiwani na watu wa Tarura.


Mwenyekiti huyo aliwaomba madiwani wenzake kutoa ushirikiano kwa wataalamu pindi wanapokuwa wanatekelezewa miradi katika kata zao wawepo ili kusimamia.


Eng Bulengela Samson ambaye ni mhandisi wa Tarura halmashauri ya Mji wa Tarime alisema yote mawazo pamoja na ushauri uliotolewa na baraza la madiwani atauchukua kwaajili ya kuufanyia kazi na yale ambayo yanahitajika kwenda kwa Meneja TARURA mkoa atayafikisha ili kufanyiwa kazi ya utekelezaji.


Mhandisi huyo alibainisha kuwa tayari wamepokea fedha shilingi milioni 650 kwa ajili ya barabara kiwango ya  kiwango cha lami kilomita moja  na kuwa wataenda kurekebisha maeneo korofi ya barabara 33 zenye urefu wa kilomota 24 na pointi katika maeneo tofauti tofauti ndani ya halmashauri ya MJI.


Diwani Viti maalumu kata ya Nyandoto m+Dorisi Maxmiliani Chacha aliuluza swala la kutaka kujua ni lini barabara za halmashauri ya Tarime mjini zitalimwa kwa kiwango na wananchi wakapata kutembea na kupita kwa urahisi bila kusumbuka.

Post a Comment

0 Comments