Kiongozi wa Kazkhastan akataa mazungumzo na waandamanaji

 


Rais wa Kazakhstan Kassym-Jomart Tokayev amekataa leo miito ya kufanya mazungumzo na waandamanaji baada ya siku kadhaa za machafuko ambayo hayajawahi kushuhudiwa, akiapa kuwaangamiza wale aliwaita kuwa ni majambazi wenye silaha. 

Katika hotuba yake leo kwa taifa, Rais Tokayev ameviamuru vikosi vya usalama vya serikali kufyatua risasi na kuuwa bila kutoa onyo. 

Aidha amemshukuru Rais Vladmir Putin wa Urusi baada ya muungano unaoongozwa na Moscow kupeleka wanajeshi wake Kazakhstan kusaidia kutuliza hali.

 Kazakhstan imeshuhudia maandamano yenye vurugu wiki hii kuhusu kupanda kwa bei za mafuta. 

Vikosi vya usalama vimeyafunga maeneo muhimu ya Almaty, ambo ni mji mkubwa kabisa wa nchi hiyo na kitovu cha machafuko ya karibuni, na vinafyatua risasi hewani kama yeyote atavikaribia.


Post a Comment

0 Comments