Ticker

6/recent/ticker-posts

Wanaotuhumiwa kula nyama za watu wakamatwa

 


Polisi Kaskazini Magharibi mwa Nigeria katika jimbo la Zamfara, wamesema kuwa wamewakamata watu wanne wanaotuhumiwa kula nyama za watu na kuuza viungo vya binadamu.


Watuhumiwa hao wamekamatwa baada ya mashushushu kukuta mabaki ya miili ya watu kwenye jengo ambalo halijakamilika ujenzi wake huku baadhi ya miili watu ikiwa haina baadhi ya viungo.


Kamishna wa Polisi wa jimbo la Zamfara, Ayuba Elkanah, amesema kubainika kwa uhalifu huo kunafuatia uchunguzi wa kupotea kwa mtoto wa kiume mwenye umri wa miaka tisa.


Watuhumiwa hao wanaume wawili na vijana wawili wa kiume walikamatwa wiki iliyopita, Kamishna Elkanah amesema na kuongeza kuwa polisi bado linawatafuta wafuasi wengine wa genge hilo.

Post a Comment

0 Comments