https://monetag.com/?ref_id=TTIb Paula Aja Kivingine Baada ya Rayvanny Kumwacha na Kurudi Kwa Fahyma | Muungwana BLOG
https://monetag.com/?ref_id=TTIb

Paula Aja Kivingine Baada ya Rayvanny Kumwacha na Kurudi Kwa Fahyma

 


Paula Kajala au Pau @therealpaulahkajala ; ni mrembo maarufu kwenye mitandao ya kijamii nchini Tanzania ambaye umaarufu wake ulipanda zaidi baada ya kuwa kwenye penzi matata na msanii Rayvanny akimchukua kutoka kwa baby mama wake, Fahyma.

Paula na Rayvanny wamekuwa kwenye mapenzi yapata mwaka mmoja sasa, lakini hivi karibuni zimeibuka tetesi kwamba jamaa huyo amerejea kwa Fahyma.


Hata hivyo, pamoja na stori hizo kuendelea kushika kurasa nyingi kwenye mitandao ya kijamii, Paula amerudi kivingine baada ya kuonesha yupo sawa na anafurahia maisha baada ya kuachia picha mpya zikimuonesha akiwa na furaha kama yote.


Baadhi ya wafuasi wake wanasema kuwa ameachia picha hizo zinazomuonesha akizidi kunoga ili kuwa kama sehemu ya kumrejesha Rayvanny kwenye himaya yake.


Kwa upande wake, Fahyma ameendelea kumrushia vijembe Paula akidai yeye ni mzuri mno na kwa sasa ameanza kunenepa baada ya kufanikiwa kumrejesha Rayvanny kwenye penzi lao.

Post a Comment

0 Comments