F Zarinah Hassan ameiomba Kampuni ya Doweicare technology limited kufanya kampeni endelevu ya ugawaji wa taulo za kike mashuleni Nchi nzima. | Muungwana BLOG

Zarinah Hassan ameiomba Kampuni ya Doweicare technology limited kufanya kampeni endelevu ya ugawaji wa taulo za kike mashuleni Nchi nzima.

 


Na Maridhia Ngemela, Mwanza.

Kampuni ya Doweicare technology limited  imetoa Pedi kwa wanafunzi   wa shule za Sekondari na msingi kwa watoto wa kike   zenye gharama ya zaidi  ya milioni 10 Mkoani Mwanza Wilaya ya Misungwi  Mei 14 mwaka 2022.


Shule 32 za Serikali  za Wilaya ya Misungwi zilizopatiwa  msaada wa taulo za kike  zipatazo  10008  na miongoni mwa shule zilizopatiwa msaada ni  Misungwi Sekondari,Milembe,Imee,Igokelo,Elpase Jitihada, na Zulu Sekondari kutoka kampuni ya Dowe soft care ikiwa na lengo la  kurudisha shukran kwa jamii na kuwasaidia watoto wa kike kuhudhuria masomo yao na kutokosa katika vipindi mashuleni ili waweze kuendelea kufanya vizuri darasani .


Balozi wa Kampuni ya Doweicare technology limited    Zarinah Hassan alipokuwa katika hafla ya ugawaji wa taulo za kike leo hii Mkoani Mwanza  Wilaya ya Misungwi   ameiomba Kampuni hiyo kuwa na kampeni endelevu ya ugawaji wa taulo zakike mashuleni ili kuwanusuru watoto hao waweze kuhudhuria vema masomo yao na kuepuka kunyanyapaliwa  ili waweze kuhudhuria  mashuleni na masomo kauli hiyo ameitoa ikiwa ni Kuelekea siku ya hedhi salama duniani ambayo hufanyika kila mwaka  Mei 28 .


Hassan amesema kuwa ,unapomsaidia mtoto wa kike kwa kumpatia taulo anakuwa na amani katika shughuli zake hata anapokuwa darasani anakuwa hana wasiwasi na anauwezo wa kuendelea kufanya vizuri katika masomo yake.


 Mkurugenzi wa kampuni ya Doweicare technology limited Victor Zangh alipokuwa akizungumza katika halfa ya ugawaji wa taulo za kike amesema kuwa, msaada huo unalengo la kurudisha shukran kwa jamii kwani wateja wa bidhaa hiyo wengi ni wanajamii hivyo ni vema kurudisha kwa jamii hususani  kwa watoto wa kike.


Zangh amesema kuwa kampuni hiyo inatambua jitihada za watoto wakike kupata elimu hivyo nawao wameamua kuunga jitihada hizo kwa kuwapatia taulo hizo ili wasikose masomo yao kwa kupata hedhi salama.


Nae mkuu wa Mkoa wa Mwanza Muhandisi Robert Gabriel aliyekuwa akizungumza kwa niaba ya Waziri wa Tamisemi Innocent Bashungwa ,amesema kuwa, tafiti  zilizotolewa na Ofisi ya Taifa ya takwimu  zinaonesha changamoto ya  hedhi salama  ni shule 66.8  huku  33.2 zikiwa  na changamoto ya hedhi salama.


Muhandisi Gabriel amesema jamii ivunje ukimwi ili kupata hedhi salama na kuondoka unyanyapaa kwa watoto wa kike na akiwahimiza wanaume wachukue hatua ya kupanga fedha ya kununua taulo za kike wa wake zao na watoto wa kike.


Sabrina Yahaya ni miongoni mwa wanafunzi waliohudhuria hafla hiyo na amesoma risala amebainisha changamoto wanazozipitia ikiwa ni pamoja  na kunyanyapaliwa mashuleni pindi wanapoingia katika siku zao za hedhi ,kukosa pesa za kununulia Pedi na wazazi kutoona umuhimu wa kuwanunulia taulo za kike.

Post a Comment

0 Comments