Madaktari wanane watafikishwa mahakamani wakishtakiwa kwa makosa ya uzembe katika kifo cha mwanasoka maarufu wa Argentina Diego Maradona.
Jaji mmoja ameamuru kusikizwa kwa kesi ya mauaji ya bila kukusudia baada ya jopo la madaktari kubaini matibabu ya Maradona yalijaa "mapungufu na kasoro".
Maradona alikufa mnamo Novemba 2020 kwa mshtuko wa moyo huko Buenos Aires, mwenye umri wa miaka 60.
Alikuwa akipata nafuu nyumbani kutokana na upasuaji wa kuganda kwa damu kwenye ubongo mapema mwezi huo.
Siku chache baada ya kifo chake waendesha mashtaka wa Argentina walianzisha uchunguzi kuhusu madaktari na wauguzi waliohusika katika uangalizi wake.
Mwaka jana, jopo la wataalam 20 walioteuliwa kuchunguza kifo chake liligundua timu ya matibabu ya Maradona ilifanya "njia isiyofaa, yenye upungufu na ya kutojali".
0 Comments