Watu wawili wauawa katika shambulizi la bunduki mjini Oslo


Polisi nchini Norway inachunguza tukio la ufyatuaji risasi uliolenga umati wa watu usiku wa kuamkia leo mjini Oslo na kusema kuwa huenda ni shambulizi la kigaidi. Watu wawili wameuawa na wengine kadhaa wamejeruhiwa. 

Kwenye taarifa yake, polisi wamesema kuwa mshambuliaji ametambulika kuwa raia wa Norway mwenye asili ya Iran na alikamatwa baada ya tukio. 

Shambulio hilo lilitokea nje ya mgahawa maarufu wa jamii ya watu wanaoshiriki mapenzi ya jinsia moja, saa chache kabla ya kuanza kwa gwaride la kila mwaka la jamii hiyo. 

Waandaji wamelazimika kusitisha tukio hilo lililopangwa kufanyika leo Jumamosi. 

Norway imekuwa nchi salama lakini imekumbwa na mashambulizi ya watu wenye misimamo mikali ya mrengo wa kulia. 

Mwaka 2011, mshambuliaji mwenye silaha aliwaua watu 69 katika kisiwa cha Utoya kilichoko mjini Oslo.


Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi