Jeshi la Mali ladai kuwaua wanamgambo 50 wakati wa operesheni


Jeshi la Mali limedai kuwaua wanamgambo 50 katika eneo la katikati mwa nchi ambako zaidi ya raia 130 waliuawa wiki moja iliyopita. 

Jeshi pia limeripoti kuwaua walinzi wawili wa kigaidi katika eneo la Mindoro pamoja na kuwakamata washukiwa nane wa kigaidi kusini mwa nchi wakati wa operesheni tofauti. 

Serikali ya Mali iliwashutumu wapiganaji wa Macina Katiba wenye mafungamano na kundi la Al-Qaeda kuhusika na mauaji ya raia katika eneo la Diallassagou na vijiji viwili jirani, mwishoni mwa wiki iliyopita. Kundi hilo lilikanusha kuhusika na mauaji hayo. 

Nchi hiyo iliyoko katika kanda ya Sahel imekumbwa na uasi tangu mwaka 2012. Machafuko hayo yalianzia eneo la Kaskazini na kisha kuenea katikati na katika nchi jirani za Burkina Faso na Niger.


Post a Comment

0 Comments