F Chama Cha Mapinduzi Mkoa Mara Wapata Viongozi Wapya | Muungwana BLOG

Chama Cha Mapinduzi Mkoa Mara Wapata Viongozi Wapya

 


Na Timothy Itembe Mara.

UCHAGUZI wa viongozi ndani ya Chama cha mapinduzi ngazi ya mkoa Mara,mgombea Christopher Mwita Ghachuma ameshinda kwa kishindo nafasi ya mjumbe wa halmashauri kuu ya Taifa NEC kwa kupata kura 750 kati ya kura 1091.


Nafasi iliyokuwa inagombewa ya mwenyekiti wa mkoa Mara  imenyakuliwa na Patrick Chandi Marwa ambaye alipata kura 635 kati ya kura zilizo pigwa 1091.


Katika uchaguzi huo mkuu wa mkoa Mara,Suleman Mzee aliwataka wajumbe wa mkutano mkuu wa uchaguzi kuchagua viongozi wenye sifa badala ya kuchagua kwa kufuata maelekezo ya watu.


Mkuu huyo alipongeza mkoa Mara kuwa umebeba sura ya kitaifa na Dunia kwa ujumla kwa hali hiyo aliwaomba wajumbe kuchagua viongozi wao kwa Amani huku wakijenga tabia ya heshima ya kumuenzi Marehemu Julius Kambarage Nyerere muasisi wa Taifa hili kwa kuzaliwa Mara.


Naye mwenyekiti mstaafu,Samwel Keboye maarufu namba 3 wakati  akifungua kikao cha uchaguzi alisema kiongozi anayeenda kuchaguliwa anatakiwa kuwa imara ambaye atakwenda kupambana na wafuasi wa vyama pinzani kwa lengo la kuhakikisha Chama cha mapinduzi kinaendelea kushika dola.


Namba 3 aliongeza kusema viongozi waliochaguliwa wanatakiwa kuiga mfano wake wa kufanya kazi ya kumsaidia Rais katika utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya Chama cha mapinduzi sio vinginevyo na yeye atakwenda kukabidhi kiti kwa kiongozi makini pindi atakapochaguliwa.


Mjumbe wa halmashauri kuu ya CCM,Ndemela Lubinga ambaye alikuwa msimamizi mkuu wa uchaguzi alipongeza watu wa mkoa Mara kumzaa na kumlea mwasisi wa Taifa  hili Rais wa awamu ya kwanza  mwalimu Julius Kambarage Nyerere na kukomboa watanzania kutoka mikononi mwa wakoloni.


Msimamizi huyo aliongeza kusema busara za mwalimu ziwekwe kwenye siasa kwa ustawi wa maendeleo ya jamuhuri Tanzanzania.


Lubinga aliwatangaza washindi wengine kuwa ni Jacob Mangaraya ambaye ni mstaafu kwa umri nafasi ya mwenyekiti UVCCM mkoa Mara.


Akihairisha mkutano huo mwenyekiti aliyechaguliwa Patrick Chandi Marwa aliwataka wanachama wa chama cha  mapinduzi kuungana pamoja ili kufanya kazi ya kuwatumikia wananchi na kuacha makundi kwasababu siasa haina uwadui bali ni kupambana kwa hoja.


Alitumia nafasi hiyo kusema ataenda kuwaunganisha na kutafuta frusa mbalimbali za kuwaunganisha kwenye mashirika ya uwekezaji wana Mara kwa ujumla.

Post a Comment

0 Comments