Iran yalaani hatua ya UN kuchunguza machafuko nchini humo

 


Wizara ya mambo ya nje ya Iran imelaani hatua ya Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa kuchunguza hatua zilizochukuliwa na Jamhuri hiyo ya Kiislamu kukabiliana na machafuko yaliyotokana na kifo cha msichana Mahsa Amini. 


Katika taarifa yake, wizara hiyo imesema inapinga azimio lililofikiwa la kuunda timu itakayochunguza maandamano hayo. 


Wizara hiyo inasema Iran tayari imeshabuni tume ya kitaifa inayojumuisha wataalam wa kisheria na wawakilishi huru. Haya yanafanyika wakati ambapo jeshi la mapinduzi la Iran limetuma vikosi vya maafisa wa usalama kuongeza nguvu katika maeneo yanayokaliwa na Wakurdi ambayo yamekumbwa na maandamano makubwa. 


Kulingana taarifa iliyotolewa na mkuu mmoja wa jeshi, hatua hiyo ni kwa ajili ya kuwazuia wale waliowaita "magaidi" kuingia nchini humo kutoka Irak.

Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi