Mke wa rais wa Ukraine Olena Zelenska: Tutavumilia


Mke wa Rais wa Ukraine Olena Zelenska ameiambia BBC kwamba Ukraine itavumilia kipindi hiki kijacho cha majira ya baridi kali licha ya ukosefu wa umeme uliosababishwa na makombora ya Urusi , na wataendelea kupigana na kile alichokielezea kama vita vya mitazamo ya dunia, kwa sababu"bila ushindi hakutakuwa na amani ".


Alikutana na mwandishi wa BBC katika mji wa kihistoria ambako kunashuhudiwa baridi kali.


Mitaa ambayo kwa kawaida huwa ina mwanagaza wa taa sasa ni giza, kutokana na ukosefu wa umeme huku Warusi wakiendelea kushambulia mitambo ya umeme ya Ukraine.


Watu wa Ukraine wameshinda majivuno kwa kusimama imara dhidi ya mashambulio ya Urusi. Lakini hili ni jaribio lingine la ujasiri.


"Tuko tayari kuvumilia hili," Olena Zelenska anasema wakati wa mahojiano akiwa katika eneo lenye ulinzi mkali ndani ya jengo lililozingirwa na mifuko ya mchanga iliyowekwa kwa ajili ya kuzuia makombora mjini Kyiv.


"Tulikuwa na changamoto nyingi sana, kuona waathiriwa wengi, kuvurugwa kwa mambo mengi, kiasi kwamba tunaona ukosefu wa umeme sio kitu kibaya zaidi kutokea kwetu." Alitoa mfano wa kura ya maoni ya hivi karibuni - 90 % ya Waukraine walisema wako tayari kuishi na ukosefu wa umeme kwa vmiaka miwili hadi mitatu iwapo wangeona matarajio ya kujiunga na Muungano wa Ulaya.


Waukraine wote watakuwa imara kwasababu ya vita hivi, alibashiri Mke wa rais wa Ukraine.

Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi