Mkurugenzi Mkuu wa RUWASA Mhandisi Clement Kivegulo ameridhishwa na utekelezaji wa mradi wa maji Igowole uliopo wilayani Mufindi Mkoa wa Iringa.
KIVEGALO na timu yake kutoka RUWASA Makao Makuu wanaendelea na ziara Mkoani Iringa ambapo wamekagua mradi huo sambamba na kutembelea Chombo cha Kutoa Huduma ya Maji Ngazi ya Jamii (CBWSO) ya SAWALA.
“Nimefurahishwa sana na utekelezaji wa huu Mradi, hawa ni baadhi ya wakandarasi wazalendo nchini, amelipwa chini ya asilimia 15 ya kazi wakati amefanya kazi kwa zaidi ya asilimia 40. Hawa ndiyo aina ya wakandarasi ambao RUWASA tunaowataka.” Alisema Kivegulo.
Mradi huo ukikamilika utanufaisha wananchi wanaoishi katika vijiji vya Ikwega, Mkalala na Igowole wapatao 19,850.
Mradi unatekelezwa na Mkandarasi kampuni ya M/S GNMS CONTRACTORS COMPANY LIMITED kwa kutumia fedha za Mfuko wa Maji (NWF) kwa Gharama ya Shilingi 3,242,561,649.15 (Bila VAT).

