Na Timothy Itembe Mara.
JESHI la polisi mkoa wa kipolisi Tarie/Rorya limefanikiwa kukamata Bunduki mbili na risasi 82 za bunduki aina ya AK-47 zilizokuwa zikimilikiwa na kutumiwa kinyume cha sheria.
"Kupatikana na nsilaha na risasi jumla ya silaha 02 zilikamatwa moja ikiwa ni Bastola aina ya Pietro Berretta yenye namba za usajili TZ CAR 76091 Pistol na ya pili ikiwa ni Short gun isiyokuwa na namba iliyokuwa imekatwa mtutu npamoja na risasi 82 za AK-47 katika msakon huo watuhumiwa 353 wamekamatwa"alisema kamandaGeofrey Sarakikya.
Kamanda huyo alibainisha kuwa jeshi hilo limefanikiwa kuwakamata na kupatikana kwa bunduki na risasi kutokana na misako iliyofanyika pamoja na elimu kwa wilaya zote sita kwa kipindi cha Julai hadi Oktoba 30 mwaka huu.
Kamanda huyo alibainisha kuwa mafanikio yamepatikana ya kesi zilizofikishwa mahakamani kama vile za uhujumu uchumi,wizi,mauaji, na unyang’anyi wa kutumia silaha kupunguza hofu ya uhalifu na wahalifu mafanikio makubwa yametokana na misako katika wilaya sita Tarime, Sirari, Nyamwaga, Kinesi, Shirati na Rorya.
Kamanda Aliongeza kuwa watuhumiwa 236 wamekamatwa wakiwa na lita 2370 za pombe haramu ya moshi,watuhumiwa 35 wamekamatwa wakiwa na kilogramu 4241 za bangi pamoja na pikipiki 09 na gari moja zilizokuwa zinatumika kusafirisha bangi na watuhumiwa 03 wamekamatwa wakiwa na mashamba ya ekari 9.5 yaliyolimwa bangi ambayo yalitekeketezwa kwa moto na kuwa wamefikishwa mahakamani ambapo watuhumiwa 06 wamekamatwa na kilo 80 za mirungi.
Katika wizi wa mifugo watuhumiwa 28 wanaojihusisha na wizi wa mifugo wamekamatwa na 20 kati yao wamefikishwa mahakamani waliobaki upelelezi unaendelea watafikishwa mahakamani wakati wowote alisema kamanda huyo.
Wengine watuhumiwa waliokamatwa ni pamoja na watuhumiwa sugu wanaojihusisha na wizi wa pikipiki unyang’anyi wa kutumia silaha uvunjaji na wizi wamekamatwa pamoja na pikipiki 04 hizo zimeibwa kutoka maeneo mbalimbali Tarime/Rorya na kwenda kuuzwa mikoa ya Geita,Mara,Mwanza,na Simiyu.
Kukamatwa kwa wavamizi na wachimbaji wa mawe wasiofuata utaratibu kuzunguka mgodi wa Barrick North Mara jumla ya viroba 2367 sawa na tani 35.5 za mawe yadhaniwayo kuwa na dhahabu vilikamatwa,kemikali aina ya mekyuri ikiwa na ujazo Gramu 200 pamoja na vilipuzi vya miamba 3 aina ya V 16 visivyo na vibali ambapo watuhumiwa 10 walikamatwa na taratibu za kisheria zinaendelea aliongeza kusema kamanda.
Katika msako huo watuhumiwa 11 wakiwemo wafanyakazi wa mgodi wa Barrick walikamatwa wakiwa na jumla ya Kilogramu 61.16 za mawe yadhaniwayo kuwa nidhahabu na kuwa watafikiishwa mahakamani baada ya taratibu za kisheria kukamilika.
Jeshi la polisi Tarime Rorya linatoa wito kwa jamii kuendelea kutoa ushirikiano kwa jeshi hilo ili kupunguza uhalifu na wahalifu pia jeshi hili linawatahadharisha watumiaji wa silaha kinyume cha sharia kuzisalimisha katika vituo husika vinginevyo mkono wa sharia utawapata wakikaidi.
