Serikali yakumbusha na kuwahimizwa wananchi wapime afya zao.


Na Ahmad Mmow, Lindi. 

 Nguvu ni mtaji wa nchi kiuchumi na maendeleo unaotokanana watu wenye afya njema ili waweze kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi. 


Hayo yalielezwa jana mjini Lindi na naibu katibu mkuu wa wizara ya nchi ofisi ya waziri mkuu sera, bunge na uratibu, Caspar Mmuya wakati wakongomano la viongozi wa dini na vijana katika siku ya pili ya wiki ya maadhimisho ya siku ya UKIMWI duniani. 


 Mmuya ambae alimuwakilisha katibu mkuu wa wizara hiyo kufungua kongamano hilo, alisema nguvu ni mtaji mkubwa wa nchi katika sekta ya uchumi. 


Kwahiyo wananchi wanatakiwa kupima afya zao kwa hiyari mara kwa mara.  Alisema kwa sasa kila palipo watu 100 ni 89.7% ya watu hao ndio wanaojua afya zao. Huku 11% wakiwa hawajui. 


Aidha Mmuya alisema 99% ya watu wanaoishi na Virusi Vya UKIMWI (VVU) wameanza kutumia dawa ya kufubaza virusi. Ambapo 96% ya watu hao walioanza kutumia dawa virusi vyao vimefubaa. 


 Kwakuzingatia takwimu hizo, naibu katibu mkuu huyo alitoa wito kwa watu wanaoishi na VVU bila kutumia dawa waanze kutumia. Kwani huduma (dawa) inatolewa bure. 


Mbali na hayo alitoa wito kwa viongozi wa dini walitupie jicho kundi la vijana. Kwani kundi hilo ndilo linaloathirika zaidi na maambukizi ya UKIMWI. 


Alisema serikali inatambua mchango mkubwa wa dini katika mapambano dhidi ya UKIMWI. Hatahivyo hazinabudi kuendelea nakazi hiyo. Hasa kwakulitupia jicho kundi la vijana. Hasa katika kutokomeza unyanyapaa. 


" Viongozi wa dini endeleeni kutoa elimu, msichoke.Viongozi mna nafasi  yakufikisha elimu,mnakutanana makundi ya aina zote," alisisitiza Mmuya. 


Kwaupande wake Shehe Hilari Shaweji Makarani (Shehe Kipozeo) alitoa wito kwa serikali kuwachukulia hatua kali za kisheria watakaobainika kuwanyanyapaa wanaoishi na Virusi Vya UKIMWI.


Nae mchungaji Richard Hananja alitoa wito kwa vijana wabadilike nakuwana  fikra za ukombozi wa kiuchumi. Kwani mambo yamebadilika. 


Huku akiweka wazi kwamba changamoto iliyopo ni vijana kuamini hakuna kazi. Lakini ukweli nikwamba changamoto ni fikra zao zinazoamini hakuna kazi wakati ukweli nikwamba wanafikiria ajira badala ya kazi ambazo zipo nyingi. 


Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi