F Uingereza inatuma helikopta nchini Ukraine kwa mara ya kwanza - Ben Wallace | Muungwana BLOG

Uingereza inatuma helikopta nchini Ukraine kwa mara ya kwanza - Ben Wallace

 


Uingereza inatuma helikopta nchini Ukraine, Waziri wa Ulinzi Ben Wallace amesema, ndege ya kwanza ya kwanza ya rubani inayopelekwa na Uingereza tangu vita kuanza.


Helikopta tatu za zamani za Sea King zitatolewa na ya kwanza tayari imewasili, BBC inaelewa.


Katika wiki sita zilizopita, wafanyakazi wa Ukraine walipata mafunzo nchini Uingereza kuzirusha na kuzikarabati ndege hizo - kutoa uwezo wa utafutaji na uokoaji.


Bw Wallace alisema Uingereza pia itatuma risasi 10,000 za ziada.


Alitoa tangazo hilo kutoka Oslo, ambapo anakutana na washirika kujadili msaada unaoendelea wa kijeshi kwa Kyiv.


Waziri huyo wa ulinzi alisema kuwa shehena hiyo ya risasi zitasaidia wanajeshi wa Ukraine kulindaeneo lililokombolewa hivi karibuni.


Ndege hiyo ya helikopta,Sea king hapo awali ilitumiwa na Jeshi la Anga na Jeshi la Wanamaji la Uingereza, na ndege ya mwisho ilistaafishwa na Jeshi la Wanamaji mnamo 2018.


Nchi chache zimetuma ndege za rubani nchini Ukraine tangu kuanza kwa mzozo huo, na maombi ya serikali yake kwa mataifa ya Magharibi kutuma ndege za kivita hadi sasa hayajajibiwa.


Mwishoni mwa wiki, Waziri Mkuu Rishi Sunak alitumia ziara ya Kyiv kutangaza awamu mpya ya msaada wa kiulinzi wa pauni milioni 50 ambao ulijumuisha bunduki 125 za kukinga ndege na vifaa vya kukabiliana na ndege zisizo na rubani zinazotolewa na Iran.

Post a Comment

0 Comments