Ukraine yazindua mpango wa msaada wa chakula kwa bara Afrika na Asia


Ukraine jana ilitangaza uzinduzi wa mpango wa msaada wa kimataifa unaoitwa ''Nafaka kutoka Ukraine," katika juhudi za kutafuta uungwaji mkono wa nchi za Afrika na Asia katika jaribio lake la kupambana na uvamizi kutoka Urusi. 


Katika mkutano na wanahabari wakati wa ziara ya waziri mkuu wa Ubelgiji Alexander de Croo, rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky, alisema kuwa "Ukraine daima imekuwa na itabaki kuwa mdhamini wa usalama wa chakula duniani" na kwamba hata katika hali mbaya ya vita, "uongozi wa Ukraine unafanya kazi kwa ajili ya uthabiti duniani". 


Zelensky amesema kuwa mpango huo utapeleka chakula kwa mataifa maskini zaidi duniani. Takriban meli 60 zitatumwa kutoka bandari za Ukraine katika bahari nyeusi karibu na Odessa, kuelekea katika mataifa kama Sudan, Yemen ama Somalia kufikia katikati ya mwaka ujao.

Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi