Bunge la chini la Urusi limepiga kura kwa kauli moja kuongeza muda wa marufuku yake dhidi ya kile kinachoitwa "propaganda ya wapenzi wa jinsia moja".
Chini ya toleo la sasa, uenezaji wowote wa mapenzi ya jinsia moja – ikiwa ni pamoja na kwa njia ya vitabu, filamu na mtandao – ni kinyume cha sheria na adhabu kali itatolewa kwa yeyote atakayepatikana na hatia hiyo.
Sheria hiyo ilipawe jina bandia la "Jibu kwa sheria ya Blinken", baada ya Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken kuikosoa kama "pigo kwa uhuru wa kujieleza".
Wanaharakati wanasema ni jaribio zaidi la Urusi la kuwakandamiza wapenzi wa jinsia moja (LGBT) wa Urusi.
Mswada wa sheria hiyo uliidhinishwa kwa kura 397 za wabunge wote wa bunge la Urusi - Duma - bila kukosa mbunge yoyote.
Mswada huo utahitaji kupitishwa na bunge la juu la Urusi kabla ya kusianiwa na Rais Vladimir Putin, lakini hili wengi wanaliona kama hatua ya kiutawala.
Toleo la awali la sheria tata ya " propaganda ya mapenzi ya jinsia moja" iliidhinishwa mwaka 2013, na kupiga marufuku "propaganda za uhusiano wa mapenzi yasiyo ya kawaida" – ikimaanisha mahusiano ya kingono ya watu wa jinsia moja – miongoni mwa watoto.
