Waasi wa M23 wasema hawatarudi nyuma DRC

 


Waasi wa M23 wanaoendesha harakati zao mashariki mwa Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Congo wamesema kuwa usitishwaji wa mapigano uliotarajiwa kuanza leo Ijumaa jioni "haulihusu " kundi hilo.


Wametoa wito kwa serikali ya Congo kufanya nao mazungumzo ya moja kwa moja.


Msemaji wa M23, Lawrence Kanyuka, amesema kuwa kwa kuwa hawakuwa na wawakilishi katika mkutano mdogo wa Jumatano uliofanyika mjini Angola, hawakujumuishwa katika mkataba.


“SisiM23 sio Warundi, sio Wanyarwanda, sio Wakenya, na wala sio Waangola. Sisi ni Wacongo , na tuko nyumbani, wanatuambia tuondoke wapi ? Tunaondoka nyumbani kuelekea wapi ?” Bw Munyarugerero anasema.


Waliotia Saini mkataba huo - kutoka Rwanda, DRC, Angola na Burundi – walisema chini ya usitishwaji wa mapigano, iwapo waasi hawataondoka katika eneo hilo kikosi cha kanda ya Afrika Mshariki kitayashambulia maeneo yao.


Serikali ya Kinshasa imekataa kufanya mazungumzo na M23, ikiwaita magaidi.


Januhuri ya kidemokrasi ya Congo, inaishutumu Rwanda kuwaunga mkono waazi, ambao wameteka eneo kubwa la jimbo la Kivu Kaskazini, mashariki mwa nchi hiyo.


Rwanda inakana kuhusika katika mzozo huo wa Congo.

Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi