Mwanamume wa California aliyefariki baada ya kugongwa na gari alionekana akisaidia bata kuvuka muda mfupi kabla ya tukio hilo, polisi wa eneo hilo walisema.
Casey Rivara, 41, alitoka kwa gari lake kabla ya kugongwa na dereva kijana huko Rocklin, karibu kilomita 40 kaskazini mashariki mwa Sacramento, polisi wa jiji walisema.
Bw Rivara alihakikisha bata wakmevuka barabara salama kabla hajagongwa kugongwa na gari, walioshuhudia walisema.
Hakuna mtu aliyekamatwa na tukio hilo.
"Mwanamume huyo aliripotiwa kusaidia kusaidia watoto wa watu walioyokuwa kwenye makutano," Idara ya Polisi ya Rocklin ilisema katika taarifa.
Summer Peterson,mmoja wa mashuhuda aliambia mshirika wa karibu wa CBS News kwamba watoto wake walishuhudia ajali hiyo, ambayo ilitokea Alhamisi mwendo wa saa mbi na robo usiku.
"Walikuwa wakisema, 'Oh, ni mzuri sana. Anafanya jambo zuri sana.' Mara ghafla akagongwa na gari, "alisema.
Watu wameweka maua na bata wa mpira katika eneo la ajali hiyo kwa heshima yake .
