Watafiti na wadau mbalimbali wa masuala ya elimu wameishauri serikali ya Tanzania kupitia upya rasimu ya mitaala ya elimu ya elimu Mei 2023 na kuonekana katika baadhi ya sera ambazo zinaonekana kutokuwa sawa kabla ya kuanza kwa utekelezaji wake.
Wanaitaka serikali itamke wazi namna ya wanafunzi pale inapotokea changamoto kwa ngazi zote za elimu.
rasimu ya sera ya elimu na mitaala tangu wadau mbalimbali wameonekana kutoridhishwa na baadhi ya baadhi katika rasimu hiyo huku wengine wakidai kuwa kuna mambo muhimu hayajazingatiwa katika kuboresha elimu ya Tanzania
Akizungumza na Sauti ya Amerika Gryson Mgoi ambaye ni kitengo cha mawasiliano katika shirika lisilo la kiserikali linalojishughulisha na masuala ya elimu la Uwezo amesema licha ya Serikali kutamka mwanafunzi aliyepata uja uzito anaweza kurudi shule lakini rasimu ya haijazungumzia chochote kuhusu kurudi shule.
Mgoi anasema kuwa:"Ilitiliwa mkazo sana kwenye sera nilitegemea liwepo ingawa limetolewa hivi karibuni la mtoto wa kike kurudi shule akipata ujauzito. Lakini ili uzito nilitegemea itamkwe kwenye sera sasa watoto wa kike watapaswa kurudi shule na ielezwe vizuri kuhusu utaratibu wa kurudi, hilo nimeona limekosekana."
Kwa upande wake Katibu Mkuu kutoka chama cha watu wenye kuishi na ulemavu, SHIVYAWATA, Jonas Lubago ametaka kamati zinazoendelea kuchambua sera kuitambua elimu iwe ni hoja katika orodha ya sera mpya huku watu wenye ulemavu zaidi ya mmoja (ambatano) watolewe tamko la wazi juu ya namna ya kuwafundisha.
Lubago anasema: “Sasa hivi wanahoja saba za sera ila tunatamani elimu iwe ni hoja ya nane ndio tuiwekee matamko yake moja kwa moja ni kwanini tunasema hivyo kuna watu wenye kuishi na ulemavu ambatano kwenye matamko ya sera pale hakuna kitu kama hicho kinachozungumzia mwenye kuishi. na ulemavu zaidi ya mmoja atafundishwa kwa mfano kiziwi, asiyeona atafundishwaje na mwalimu kwa idadi ya wanafunzi haijazungumzwa kwa yule ni mwanafunzi mmoja anahitaji mwalimu mmoja.
Hata hivyo Michael Kamukulu ambaye ni mtafiti wa masuala ya elimu nchini ameishauri serikali kuangalia mfumo wa motisha katika rasimu ya sera waliouweka kwa motisha unatolewa baada ya kuonekana matokeo na mabadiliko.
Kamukulu anaeleza: “Mfumo wa motisha inabidi uzingatiwe pia bahati nzuri tumekuwa na tafiti nyingi unaweza ukatoa motisha tena kubwa kabisa lakini mwisho wa siku matokeo yakawa ni yale tunashauri unapoahidi aonyeshe mabadiliko ndio umpe motisha sio malipo tuite bakishishi kinachompoza baada ya matokeo kuwepo. .”
Ikumbukwe rasimu mpya ya Sera ya Elimu na Mafunzo, iliwasilishwa bungeni Dodoma katika fedha ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Mei 16, 2023 ambapo wizara inaendelea kupokea maoni kuhusu sera hiyo hadi Mei 31, 2023 na Juni mwaka huu wizara kuomba idhini ili kuwezesha. utekelezaji wake.