Wakazi wa Kijiji cha Sunuka Uvinza mkoani Kigoma, kwa kushiriki na serikali ya kijiji hicho, wamelazimika kuchukua waganga wa jadi zaidi ya 10 kutoka Sumbawanga ili kukagua watu wanaofanya uchawi wakidai kuwa chanzo cha vifo vya vijana katika mazingira ya kutatanisha.
Waganga hao wamepewa dhamana hiyo ya kusaka wachawini hapo ambapo wananchi walifika mpakani mwa kijiji cha Rulinga kuweka vizuizi kwa Mkuu wa wilaya ya Uvinza Dinah Mathamani asiingie katika kijiji Chao wakihofia atazuia oparesheni hiyo.
Katika mkutano huo Mkuu wa wilaya ya Uvinza Dinah Mathamani ametoa maagizo ambayo yamekataliwa na wananchi, kwa madai kuwa suala hilo halipo kisheria na hata serikali haiamini licha ya wananchi wakihitaji atoe kibali cha kuendelea na zoezi hilo la kusaka wachawi .
Hatua ya kukosekana makubaliano, inailazimu kamati ya kurudi nyuma nyuma vijiji viwili Ilagala na suala hilo kisha kutoa tamko rasimi ambapo Mkuu wa Wilaya ya Uvinza, ameagiza waganga hao waondoke mara moja la sivyo sheria itawahusu wakiwepo pia viongozi wanaotoa kibali cha usaka wachawi.
Tetesi zinasema, ili zoezi zoezi hilo, wananchi wanachangishwa shilingi elfu tano kuwezesha oparesheni hiyo, ikipata baraka kutoka serikali ya kijiji, licha ya viongozi wa Kijiji akiwemo mwenyekiti Hamisi Idi na Diwani hawakuweza kutokea mkutanoni.
