F Wakazi wa Dodoma waendelea kuupiga mwingi na Airtel na kujishindia zawadi | Muungwana BLOG

Wakazi wa Dodoma waendelea kuupiga mwingi na Airtel na kujishindia zawadi


WAKAZI saba wa Mkoa wa Dodoma wameibuka kidedea na kujishindia  zawadi mbalimbali kupitia promosheni  kabambe  ya ‘Upige Mwigi na Airtel imeelezwa.

Promosheni hii ya miezi mitatu ya Kampuni inayoongoza katika kutoa huduma za simu za mawasiliano nchini ya Airtel ambayo washindi wake wanapatikana kwa kutumia huduma ama kufanya miamala ya Airtel Money, inashuhudia wateja wa kampuni hiyo wakijizolea zawadi lukuki za pesa taslimu, television, pikipiki, muda wa maongezi na majokofu, Airtel ikitenga pesa jumla ya shs milioni 250 kuifanikisha.

Akizungumza kaika hafla ya kukabidhi zawadi kwa washindi wa television na majokofu kwa wakazi wa Dodoma jana, Mkurugenzi Mkuu wa Mawasiliano wa Airtel Tanzania, Beatrice Singano alisema promosheni hiyo ni ya kipekee kwani kila mteja ama wakala anaweza kuwa mshindi.

 “Wateja na mawakala wanaweza kujishindia zawadi za hapo kwa papo kama vile muda wa maongezi, pikipiki, jokofu, fedha taslimu kuanzia milioni moja mpaka milioni 50 kila siku.
 

“Zaidi ya zawadi hizo pia Airtel imeongeza sababu  nyingine ya kutabasamu kwa wateja wetu kwani sasa wateja wote wa Airtel wanaweza kuangalia salio la akaunti za za Airtel money bila makato”, alisema Bi. Singano akiongeza kuwa kwa mteja anayefanya miamala mingi ana nafasi kubwa ya kushinda zawadi na kwa  mawakala halikadhalika.

Akizungumza katika hafla hiyo, Mkuu wa Mauzo wa Airtel mkoani humo, Salum Ngululu alisema ili kushiriki mteja anahitaji kufanya miamala kwa kutumia menu ya kawaida ya *150*60# au kutumia aplikesheni (app) ili aweze kuingizwa katika droo na kujishindia zawadi.

“Mpaka mwisho wa promosheni hii jumla ya washindi 90 watajishindia zawadi ya shs milioni moja, washindi 48 wa majokofu ya milango miwili  kila wiki , televisheni ya inchi 55, washindi wawili wa pikipiki katika droo ya mwezi na mwisho mteja wetu mmoja ataibuka na shangwe la zawadi ya shs milioni 50.

“Airtel inaendelea kuupiga mwingi pamoja na wateja wake ikiwa imesambaza huduma zake kote nchini na kufungua maduka maalumu ya Airtel money branch zaidi ya 3500 na wakala zaidi ya 2000 huku ikiendelea kuwekeza katika kupanua mtandao wa 4G kwenye minara yake yote na kuwafikia watanzania wote hasa waishio maeneo ya vijijini”, alisema Bwana Ngululu.

Akipokea zawadi yake ya television,  mkazi wa Dodoma Thabiti Hemedi aliishukuru Airtel kwa zawadi hiyo licha ya kutoitarajia hivyo akawataka wateja wengine kuupiga mwingi na Airtel ili washinde zawadi kama yake kwani zawadi zinatolewa bila mchongo.

Mshindi mwingine aliyejinyakulia jokofu, Silvano Chigwaye  naye pamoja na kuishukuru Airtel lakini pia kama Hemedi alisema zawadi zote zinazotolea na kampuni hiyo kupitia promosheni zake ni za kweli na za bila upendeleo.

Katika wateja hao saba, washindi walioshinda televisheni ni Piston Benjamin, Emannuel Funto, na Thabiti Hemedi, huku Juma Mafita, Silvano Chigwaye na Hezron Masigose wakijishinda majokofu za zawadi ya pesa taslimu shs milioni moja ikienda kwa Joseph Mahumba.



Mkuu wa Mauzo wa Kampuni ya Simu za Mkononi wa Airtel Tanzania Mkoa wa Dodoma, Salum Ngululu (katikati), akikabidhi zawadi ya jokofu kwa mkazi wa Dodoma, Silvano Chigwaye ambaye ni mmoja wa washindi  wa promosheni inayoendelea ya Upige Mwingi na Airtel katika hafla iliyofanyika mkoani humo mwishoni mwa wiki. Kushoto ni Mkuu wa Mawasiliano wa Airtel Tanzania, Beatrice Singano.

Post a Comment

0 Comments