KUELEKEA Msimu wa Sikukuu za Chrismas na Mwaka mpya Kampuni ya Startimes imezindua rasmi Kampeni ya "Lipa tukubusti" itakayodumu miezi mitatu kuwaweka karibu watazamaji kiburudani na kimichezo.
Akizungumza na Wanahabari Leo Novemba 20,2023 Meneja Masoko wa Kampuni ya Startimes David Malisa amesema msimu huu wa Sikukuu familia zinakuwa pamoja hivyo Kampeni hiyo itawapa nafasi ya kupata ofa kabambe ya kifurushi cha juu mara baada ya kulipia kifurushi chochote kile ikiwemo Nyota , Uhuru,Mambo ,Smart pamoja na Super.
Hata hivyo Malisa ameongeza kuwa watuamiaji wa 'Startimes on' wataweza kupata ofa hiyo kwa wale ambao watakuwa wameunganisha moja kwa moja na visimbuzi vyao.
"Visimbuzi vyetu pia tumevishusha bei ambapo Antena unaweza kukipata kwa bei ya elfu 25000 huku Kisimbuzi full seti inapatikana kwa shilingi elfu 40000 na ukipata ofa ya kupandishwa kifurushi cha juu yake huku atakaeweza kununua Kisimbuzi cha dishi elfu 56000."
Pia ameongeza kuwa msimu wa Kampeni hiyo imeongeza chaneli tatu zenye maudhui tofauti tofauti ikiwemo ingizo la chaneli mpya yenye maudhui ya katuni ya watoto "Boing" pamoja na Discovery na TLC.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa vipindi kutoka Tv3 Emmanuel Sikawa ameongeza kuwa wamejipanga vizuri kuendelea kutoa maudhui ya kimichezo ambapo chaneli hiyo imebeba maudhui ya kimichezo 75% huku 15% ni mtindo wa maisha ( Life style).
''Bado tunaendelea kuonesha michuano ya mipira daraja la kwanza (NBC Championship) tv3 imekuwa ikirusha mechi 6 kila wiki ambapo tayari mechi 61 zimeoneshwa kati ya mechi 88. Kwa picha angavu".
Pia amesema watu wa Dar wategemee kipindi kipya cha mdahalo wa kimichezo (Football Breakfast) hivi karibuni amabapo watashirikishwa wanamichezo nguli na viongozi wa Serikali kuchambua michezo mbalimbali ikiwemo soka,ngumi na riadhaa.
0 Comments