VIDEO: Airtel na Itel yatambulisha Simu mpya na zawadi ya GB 75 bure


Kampuni ya Mtandao wa Simu ya Airtel Tanzania kwa kushirikiana na Kampuni ya Simu ya Itel imeitambulisha rasmi Simu mpya aina ya Itel A70 ikiwa na uwezo wa kipekee ikiwemo Memori ya 8GB+128GB, betri yenye nguvu ya 5000mAh, fingerprint na chaji ya TYPE-C zitakazofanya mtumiaji kufurahia simu yake.

Akizungumza baada ya utambulisho wa Simu hiyo uliofanyika jijini Dar es Salaam, Meneja wa Uhusiano wa Airtel Tanzania Jackson Mbando amesema Airtel imejipanga kushirikiana na wadau katika kusogeza huduma bora kwa watanzania, inayoendana na mabadiliko ya teknolojia na kuiunga mkono serikali kwenye mapinduzi ya kidigitali.

Amesema kuwa kuputia ushirikiano huo, Airtel Tanzania itatoa ofa ya GB75 za kuperuzi mwaka mzima ukiwa na mtandao wa Airtel kwa atakayenunua simu ya itel A70 ambayo kwa sasa inapatikana katika maduka yote ya simu nchi nzima.

TAZAMA FULL VIDEO HAPA CHINI.......USISAHAU KUSUBSCRIBE 

Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items