VIDEO: Mfanyakazi wa Posta akamatwa na mafuvu ya fisi Airport Dar


Jeshi la Polisi Kikosi cha Viwanja vya Ndege Aprili 23, 2024 walimkamata Harold Eliamringi Urio, mfanyakazi wa shirika la Posta akisafirisha boksi lililokuwa limetumwa na Issa Ajali Likwembe mkazi wa kimara Dar es salaam kwenda kwa Ben Williams wa Burnley Engand likiwa na mafuvu manne ya wanyamapori aina ya Fisi, vichwa kumi vya ndege aina ya Kwarara /BIS (vitano vya glossy Ibis na vitano vya Hadada Ibis) pamoja na mafuvu matatu ya wanyamapori aina ya Pimbi.

TAZAMA FULL VIDEO HAPA CHINI.......USISAHAU KUSUBSCRIBE 

Post a Comment

0 Comments