Na John Walter -Babati
Timu ya Fountain Gate FC imewasili salama mjini Babati ikitokea mkoani Tabora katika mchezo wao dhidi ya Tabora United.
Timu hiyo imepata mapokezi makubwa kutoka kwa Mashabiki wao baada ya kuwafurahisha kwa kuwachapa Tabora United mabao 3-1 Jana mjini Tabora.
Mamia ya Wananchi wa mji huo walilipuka kwa shangwe kubwa huku barabara kwa muda kwa bajaji na pikipiki.
Mashabiki hao wakiongozwa na wale wanaounda TAWI la Fountain Gate royal fans Babati walizunguka mitaa mbalimbali wakiwa na wachezaji pamoja na Viongozi wa timu hiyo wakionesha kufurahishwa na mwenendo wa kikosi hicho.
Hata hivyo uongozi wa Fountain Gate FC umethibitisha kuwa wataendelea kuweka makao yake mjini Babati na kutoa burudani nzuri ya kabumbu safi.
0 Comments