Mkurugenzi wa Mati Aonyesha Helikopta Yake Mpya kwa Umma



Na John Walter -Babati 

Mkurugenzi wa Kampuni ya Mati, ambaye pia ni mmoja wa wafanyabiashara maarufu nchini, ameonesha kwa mara ya kwanza helikopta yake mpya leo.

Helikopta hiyo, ambayo imekuwa gumzo, ilitua katika Uwanja wa Tanzanite Kwaraa uliopo Mjini Babati Mkoani Manyara, huku wananchi wakijitokeza kwa wingi kushuhudia tukio hilo la kihistoria.

Mkurugenzi huyo alifika na familia yake akitokea Dar es Salaam, akieleza kuwa lengo la kumiliki helikopta hiyo ni kurahisisha safari zake za kikazi na kibiashara, hususani katika maeneo yenye changamoto za miundombinu.

“Tumeona ni muhimu kuwa na usafiri wa haraka na wa uhakika ili kuboresha utendaji wa shughuli zetu, hasa katika maeneo ya vijijini ambako huduma za anga ni msaada mkubwa,” alisema Mkurugenzi huyo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari.

Wananchi waliojitokeza walionekana kufurahia tukio hilo, huku wengine wakieleza kuwa hatua hiyo inaonyesha maendeleo na uwekezaji mkubwa unaofanywa na wafanyabiashara wa ndani.

Ni matarajio ya wengi kuwa Helikopta hiyo itasaidia katika shughuli mbalimbali za dharura, ikiwemo usafirishaji wa wagonjwa na usaidizi wa kiufundi katika maeneo ya mbali.

Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi