Na.Mwandishi wetu Arusha .
Zaidi ya waoneshaji 500 kutoka nchi 13 Mawakala wa Usafiri zaidi ya 800 kutoka nchi zaidi ya 40, na wageni wapatao 15,000, wanatarajiwa kuhudhuria maonesho makubwa ya utalii mashariki mwa Afrika Karibu -Kilifair 2025 yatakayofanyika jijini Arusha Juni 6 hadi 8,2025.
Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Arusha ,Mkurugenzi wa KKF Bwana Dominic Shoo alisema kuwa KARIBU-KILIFAIR ni jukwaa kuu kwa waoneshaji zaidi ya 500 kuonyesha bidhaa zao.”.
Bw.Shoo alisema kuwa,KARIBU-KILIFAIR ni tukio kuu la utalii Afrika Mashariki na ni matokeo ya kuunganishwa kwa maonesho mawili makubwa ya utalii nchini Tanzania.
"Mwaka huu tumepanua eneo la maonesho kufikia mita za mraba 40,000 katika viwanja vya Magereza, Arusha,Kwa kuzingatia viwango vya kimataifa, ubunifu mpya na mpangilio wa wazi, KKF imejijengea heshima kubwa kama jukwaa bora la biashara ya utalii."Alisema Shoo.
Bw.Shoo alisema kuwa Kampuni ya KILIFAIR Promotion Company Ltd inazindua toleo la 10 la maonesho ya utalii ya KARIBU-KILIFAIR (KKF) ambapo maonesho ya mwaka huu yana utofauti mkubwa kwani yameboreshwa.
" Tumepanua eneo la maonesho kufikia mita za mraba 40,000 katika viwanja vya Magereza, Arusha,kwa kuzingatia viwango vya kimataifa, ubunifu mpya na mpangilio wa wazi, KKF imejijengea heshima kubwa kama jukwaa bora la biashara ya utalii."Alisema
Nae Mkurugenzi Mtendaji KKF bw.Tom Kunkler alisema kuwa maonesho ya mwaka huu yamelenga utalii endelevu ndani ya Karibu -Kilifair ,ambapo kwa kulenga mustakabali wa mazingira, wameanzisha mpango wa “Uendelevu wa Utalii” kwa kutumia vifaa vya mbao, vibuyu vya maji, utenganishaji wa taka na maeneo ya kuchakata chupa. Haya ni baadhi tu ya hatua kuelekea maonesho ya kijani ya siku zijazo.
Alisema kauli mbiu ya mwaka huu ni “Biashara hukutana na Wanyamapori” inathibitisha kuwa Tanzania ni kituo bora cha MICE (Mikutano, Maonyesho, Mikutano ya Kitaaluma, na Matukio) ambako biashara na burudani vinakutana."
Bw.Tom alisema kiingilio kwa watu wazima ni shs 10,000 kwa watu wazima na 5,000 kwa watoto hivyo ametoa wito kwa wadau mbalimbali kujitokeza kwa wingi kuja kujionea vitu vya tofauti katika maonesho hayo ."Alisisitiza Tom
Hata hivyo Serikali ya Tanzania inayoongozwa na Mhe. Rais dkt.Samia Suluhu Hassan imeipa kipaumbele sekta ya utalii kupitia kwa Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Pindi H. Chana, ambaye amekuwa akitangaza vivutio vya Tanzania duniani kote na Serikali imeitambua rasmi KARIBU- KILIFAIR kama jukwaa muhimu la masoko ya utalii kupitia pia matukio kama “My Tanzania Roadshows” na “Z-Summit” ya Zanzibar.
0 Comments