Na John Walter -Babati
Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Babati Vijijini na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Daniel Sillo, ameibuka mshindi katika mchakato wa kura za maoni ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), baada ya kupata kura nyingi katika kata zote 25 za jimbo hilo, na hivyo kusalia kuwa chaguo la wajumbe kupeperusha bendera ya chama hicho katika uchaguzi mkuu wa Oktoba 2025.
Daniel Sillo alipata ushindi wa kishindo katika kata kwa kura 9,056 huku anayefuatia Emmanuel Gekul akiwa na kura 2,426, jambo lililodhihirisha kuwa bado anaungwa mkono na wanachama wa CCM na wananchi kwa ujumla.
Ushindi huo unamuweka Sillo kwenye nafasi nzuri ya kuwania tena ubunge kwa kipindi cha pili mfululizo, huku akitegemewa kuendeleza utekelezaji wa miradi ya maendeleo, uboreshaji wa huduma za jamii, na kuimarisha usalama wa wananchi wa Babati Vijijini kupitia nafasi yake ya serikalini.
0 Comments