F Emmanuel Khambay aongoza kura za maoni Babati mjini. | Muungwana BLOG

Emmanuel Khambay aongoza kura za maoni Babati mjini.

 


Na John Walter-Babati

Mgombea mpya katika kinyang'anyiro cha ubunge wa Jimbo la Babati Mjini kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Emmanuel Khambay, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi wa CCM Wilaya ya Babati Mjini, ameibuka na ushindi wa kishindo katika kura za maoni zilizofanyika hivi karibuni.
Khambay, ambaye alikuwa akiwania nafasi hiyo kwa mara ya kwanza, amewashangaza wengi kwa kupata kura nyingi kutoka kwa wajumbe wa chama katika kata zote nane za jimbo hilo, jambo linaloonesha kukubalika kwake kwa kiwango kikubwa.
Ushindi wa Khambay umechangiwa zaidi na sera zake zenye mashiko, zinazolenga kuleta maendeleo jumuishi, kutetea maslahi ya wananchi wa Babati Mjini na kushirikisha vijana na makundi yote katika ajenda ya maendeleo.
Wajumbe wengi walieleza kuvutiwa na maono mapya ya kiongozi huyo kijana, ambaye licha ya kuwa mgeni katika kinyang'anyiro cha ubunge, ana rekodi nzuri ya uongozi ndani ya chama na jamii kwa ujumla.
Mchakato huu ni sehemu ya maandalizi ya CCM kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2025, ambapo chama hicho kinaendelea kuchuja na kuchagua wagombea bora watakaoweza kushindana katika uchaguzi na kutekeleza ilani ya chama kwa ufanisi.

Post a Comment

0 Comments