Na John Walter-Mbulu
Festo Banga Bayyo ameibuka mshindi katika mchakato wa kura za maoni ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa nafasi ya ubunge wa Jimbo la Mbulu Vijijini, baada ya kuzoa jumla ya kura 5,706, na kuwaacha wapinzani wake kwa tofauti kubwa ya kura.
Katika mchakato huo uliohusisha wajumbe wa CCM kutoka maeneo mbalimbali ya jimbo hilo, Banga Bayyo aliongoza mbele ya wagombea wengine wanne waliokuwa wakichuana kuwania tiketi ya chama hicho kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu ujao.
Matokeo kamili ya kura za maoni yalikuwa kama ifuatavyo:
Festo Banga Bayyo – 5,706 kura
Emmanuel Qambaji Nuwas – 3,165 kura
Grace Saulo Mali – 1,484 kura
Bahati Samwel Sulle – 158 kura
Samwel Gidaguda Malleyeki – 128 kura
Mchakato huu ni sehemu ya maandalizi ya CCM kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2025, ambapo chama hicho kinapitia kura za maoni kuchagua wagombea wake wa nafasi mbalimbali za uongozi.
Wakati ukisubiriwa uamuzi wa mwisho kutoka Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM (NEC), jina la Festo Banga Bayyo sasa linaonekana kuwa na nafasi kubwa ya kupeperusha bendera ya chama hicho katika kinyang’anyiro cha ubunge wa Mbulu Vijijini.
0 Comments