F Matokeo ya ubunge viti Maalum mkoa wa Manyara | Muungwana BLOG

Matokeo ya ubunge viti Maalum mkoa wa Manyara

Na John Walter-Babati

Msimamizi wa Uchaguzi Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Jabir Shekimweri, amewatangaza Regina Ndege na Yustina Rahhi kuwa washindi wa nafasi ya Ubunge wa Viti Maalum kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Manyara.

Regina ametangazwa mshindi baada ya kujizolea kura 891 na Yustina Rahhi kura 705 kati ya zaidi ya kura 1109 zilizopigwa na wajumbe waliokuwa wakishiriki uchaguzi huo uliofanyika leo Julai 30, 2025, katika ukumbi mpya wa CCM Mkoa wa Manyara uliopo mjini Babati.

Wajumbe walikuwa 1067, Kura halali zilikuwa 1099 ikijumuisha makundi ya viongozi na wagombea ,kura 10 ziliharibika.

Jumla ya wagombea katika uchaguzi huo walikuwa nane.

Matokeo kura za Maoni UWT Mkoa wa Manyara.

Anna Shinini 23
Scholar Mollel  37
Paulina Nahato 71
Loema Peter 90
Joseline Umbulla 168
Sinorina Jorojick  214
Yustina Arkadius Rahhi 705
Regina Ndege Qwaray 891

Post a Comment

0 Comments